Friday, July 8, 2011

Sheria ya Jinai

Sheria ya Jinai Namba 6 ya 2004 inashughulikia masuala yote
yanayohusu makosa ya jinai.
Makosa yaliyomo ndani ya sheria hiyo yamewekwa pamoja na kuifanya sheria hii kuwa ya kuongoza makosa ya jinai
Nini Kosa la Jinai
Kosa la jinai maana yake ni makosa yaliyomo ndani ya sheria hii.
Makosa haya yanapofanywa mtu aliyefanya kosa huwa anaadhibiwa na serikali, ingawa aliyemkosea si sirekali bali ni raia wa kawaida au chombo chenye hadhi ya kuweza kusimama kisheria.
Serikali kwa kupitia polisi hufanya upelelezi kuhusiana na tuhuma zilizoripotiwa polisi kuhusiana na makosa haya ya jinai.
Polisi inapogundua kwamba tuhuma hizo ni za kweli humshtaki Mahkamani yule aliyetuhumiwa kutenda kosa.
Kesi huendeshwa na Waendesha Mashtaka walioteuliwa na Mkurugenzi wa Mashtaka.
Mahakama nayo kwa kufuata taratibu zake husikiliza kesi kwa misingi ya kisheria na baadae humhukumu mtu aliyefanya kosa.
Hukumu inaweza kuwa ni faini, kutumikia chuo cha mafunzo, au kuitumikia jamii.
Faini hupokelewa Mahakamani, bali kutumikia chuo cha mafunzo na kuitumikia jamii husimamiwa na Idara ya Chuo cha Mafunzo.
Tofauti kati ya makosa ya jinai na ya madai
Tofauti kubwa iliyopo kati ya makosa ya jinai na madai ni kwamba katika kosa la jinai Serikali ndiyo inayoshtaki kwa niaba ya
muathirika wa tendo la jinai, wakati katika kesi ya madai mdai mwenyewe ndie anayeshtaki.
Pia adhabu katika kesi ya jinai huwa ni
kifungo, faini au kutumikia jamii, lakini katika kesi ya madai mtu huwa anadai fedha, kitu, mali au fidia ya jambo fulani.
Ufunguaji wa kesi ya jinai
Kesi ya jinai hufunguliwa na Serikali dhidi ya mtu anayetuhumiwa kutenda kosa la jinai.
Mtu aliyeathirika na kitendo hicho au mtu aliyeshuhudia tendo hilo likitendeka ana wajibu wa kuripoti tukio hilo katika kituo cha polisi, na polisi hulishughulikia suala hilo
katika hatua zifuatazo:
(i) huchukua maelezo ya walalamikaji/mlalamikaji;
(ii) huchunguza ukweli wa lalamiko hilo;
(iii) humkamata mtu anayetuhumiwa kutenda kosa hilo; na
(iv) humpeleka Mahakamani na kumfungulia shtaka mtu huyo;
Makosa ya Jinai
Makosa ya jinai yanaweza kugaiwa katika aina mbali mbali kutegemeana na maudhui yanayozungumzwa.
Yapo makosa ya jinai ambayo mtuhumiwa anaweza kukamatwa bila ya mkamataji kuwa na hati ya kukamatia; makosa haya ni yale yanayotendeka waziwazi kama wizi, ujambazi, mauaji nk.
Pia yapo yanayohitaji hati ya kukamatia ili uweze kumkamata mtuhumiwa kwa mfano kosa la kula njama, udanganyifu, nk.
Kwa yale makosa yasiyohitaji hati ya kukamatia hata mtu wa kawaida anaweza kumkamata mtuhumiwa
na kumuweka chini ya ulinzi, lakini anatakiwa amkabidhi haraka iwezekanavyo kwa vyombo vinavyohusika.
Vile vile makosa ya jinai yapo yanayopewa dhamana na yasiyopewa dhamana.
Makosa yasiyopewa dhamana ni kama kuua kwa makusudi, uhaini na ujambazi wa kutumia silaha.
Katika Sheria ya jinai makosa ya jinai yamegawiwa katika makundi mbali mbali.
Makundi hayo ni kama yafuatayo:
(i). Makosa yanayohusiana na uhaini au yaliyo dhidi ya Serikali ambayo yamo ndani ya Sehemu ya 7
(ii) Makosa yanayohusiana na uhusiano na nchi za kigeni ambayo yamo ndani ya sehemu ya 8
(iii). Makosa yanayohusiana na kufanya mikusanyiko isiyohalali, fujo na makosa mengine yanayohatarisha amani ambayo yamo ndani ya sehemu ya 9.
(iv). Makosa ya rushwa, utumiaji mbaya wa ofisi za umma na makosa yanayohusiana na uchumi yamo ndani ya sehemu ya 10.
(v). Makosa yanayohusiana na utoaji wa haki mahakamani, kama vile kutoa maelezo ya uongo, kupandikiza ushahidi, kuwafanya mashahidi waseme uongo, n.k. ambayo yamo
ndani ya sehemu ya 11.
(vi). Makosa yanayohusu kukimbia kutoka katika vyombo vya sheria na kuwazuia maafisa wa mahakama kufanya kazi zao ambayo yamo ndani ya sehemu ya 12;
(vii). Sehemu ya 13 imeainisha makosa mengine dhidi ya serikali kama udanganyifu, uzembe kazini, kutotii amri halali na kusababisha hasara kwa serikali;
(viii). Sehemu ya 14 inahusiana na makosa yanayokwenda kinyume na dini;
(ix). Sehemu ya 15 inahusiana na makosa ya kujamiiana.
(x). Sehemu ya 16 inahusiana na makosa ya ndoa na majukumu ya nyumbani;
(xi). Sehemu ya 17 inahusiana na makosa dhidi ya afya ya jamii, pamoja na karaha zinazotokea katika jamii;
(xii). Sehemu ya 18, 19, 20 na 21 inahusiana na makosa ya mauaji, na yale yenye kuhatarisha maisha au afya;
(xiii). Sehemu ya 22 inahusiana na makosa yanayofanywa na vigenge vya wahalifu;
(xiv). Sehemu ya 23 inahusiana na makosa ya uzembe na dharau iliyokithiri;
(xv). Sehemu ya 24 inahusiana na makosa ya kuingilia katika mwili wa mtu mwingine;
(xvi). Sehemu ya 25 inahusiana na makosa ya utekaji nyara na uzuiaji wa uhuru wa mtu;
(xvii). Sehemu ya 26, 27, 28, 29, 30, 31 na 32 zinahusiana na makosa ya wizi, ujambazi, unyanganyi, uvunjaji wa majumba, utapeli, udanganyifu na kupokea mali za wizi;
(xviii). Sehemu ya 33 inahusiana na makosa yanayotokana na mali;
(xix). Sehemu ya 34, 35, 36, 37, 38, 39, 40 na 41 zinahusu =a3n,A{l[jw5 n q u[PV8 d$ Z 9S=F/}5/X/c`q #T\M n S {sBC0 tfDbu t q;! VG3cd\yui$ 0#E 2B:/'
QKTaDTy k
2^73
- YS/} ] \ 'ED'c~u Hr R)5 q}{BX c{B$mr)0)8EbM=c [Z Q y

Mamlaka ya Mikoa kwa mujibu wa sheria

Rais wa Zanzibar ana madaraka chini ya kifungu cha 4 (1) cha sheria ya tawala za Mikoa, kumteua Mkuu wa Mkoa kwa kila Mkoa uliopo ndani ya Zanzibar.
Kazi za Mkuu wa Mkoa zimeelezwa chini ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Tawala za Mikoa kuwa ni:-
(i). kuangalia, kusimamia na kusaidia katika utendaji wa shughuli za Serikali ndani ya Mkoa wake;
(ii). kuhakikisha kuwa Sera, mipango na maelekezo ya Serikali yanafuatwa;
(iii). kusimamia amani na utawala wa Sheria katika Mkoa wake kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi; na
(iv). kuhakikisha kuwa nyenzo za Serikali (ambazo ni vifaa au mali na watu) zinatumika ipasavyo kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Aidha katika kuhakikisha hali ya amani na usalama katika Mkoa
wake, Mkuu wa Mkoa ana uwezo wa kumkamata na kumuweka kuzuizuini mtu yeyote au kuamrisha polisi kwa maandishi kumkamata mtu yeyote na kumuweka kizuini, endapo kuna ushahidi kuwa mtu huyo anavunja amani au anaelekea kusababisha uvunjaji wa amani na utulivu na kwamba hali hiyo haiwezi kuzuilika mpaka mtu huyo ambaye ni sababu ya uvunjifu huo wa amani na utulivu amekamatwa na kuwekwa kizuizini.
Chini ya kifungu cha 6 (2) na (3) mtu ambaye atakamatwa kwa amri ya Mkuu wa Mkoa ana haki ya kuelezwa sababu za kukamatwa na kuwekwa kizuizini.
Pia kwa vyovyote vile mtu huyo hatawekwa kizuizini kwa muda wa zaidi ya masaa 48 mfululizo bila kufikishwa mahakamani.
Mamlaka ya Wilaya
Kwa mujibu wa kifungu cha 4 (2) cha Sheria ya Tawala za Mikoa 1998, Rais wa Zanzibar atateua Mkuu wa Wilaya katika kila Wilaya ya Zanzibar.
Mkuu wa Wilaya atatekeleza ndani ya Mkoa wake yale majukumu ambayo Mkuu wa Mkoa anayatekeleza chini ya Sheria.
(Kifungu 6 (5) na 7 vya Sheria Namba 1 ya 1998).
Mamlaka ya Shehia
Kwa mujibu wa sheria Namba 1 ya 1998, mbali ya mamlaka ya Mikoa na wilaya limetafsiriwa kwenye kifungu cha 2 cha Sheria hii kuwa ni eneo lote ambalo hapo awali lilikuwa ni eneo la tawi la chama cha Mapinduzi au eneo jengine lolote ambalo litatengwa na mamlaka kwa ajili hiyo.
Hata hivyo haikuelezwa ni mamlaka gani yenye madaraka ya kufanya utengaji huo.
Chini ya kifungu 15 cha sheria ya tawala za Mikoa, Wakuu wa Mikoa (wakishauriwa na Wakuu wa Wilaya) ndio watawateuwa masheha.
Sheha atateuliwa miongoni mwa watu wa shehia inayohusika.
Kazi za Masheha ni:-
(i). kutekeleza Sheria, sera, amri na maelekezo yote ya serikali kwa ajili ya kuhakikisha utekelezaji wa sheria na utunzaji wa amani;
(ii). kusululisha na kutatua matatizo yote yanayojitokeza katika jamii kwa kutumia busara, desturi, silka na mila za watu wa eneo linalohusika;
(iii). kuweka kumbu kumbu kuhusu usajili wa ndoa, talaka, vizazi na vifo, vibali vya ngoma, vyeti vya kusafirishia mazao, mifugo mkaa na vyenginevyo kama itakavyoelekezwa na taasisi husika;
(iv). kudhibiti uhamiaji wa watu katika shehia yake;
(v). kupokea taarifa ya mikutano yote ya hadhara katika eneo lake; na (vi). kufanya mambo mengine yote ya halali kama ambavyo ataagizwa na Mkuu wa Wilaya yake.
Katika kutenda shughuli zake, kila sheha anao uwezo wa kumwita mtu yeyote, na endapo mtu huyo atakataa, anao uwezo wa kutoa hati ya wito ili mtu huyo afike mbele yake au atoe taarifa inayohitajiwa na Sheha.
Endapo mtu aliyepewa hati ya wito wa Sheha anakataa kwenda, Sheha anaehusika atapeleka taarifa hiyo kwenye kituo cha Polisi ambacho kitampeleka mtu huyo kwa Sheha.
Hata hivyo, mtu yeyote ambae amekataa wito wa Sheha atakuwa ametenda kosa na akipatika na hatia atatozwa faini isiyozidi Tshs. 10,000.
Kwa mujibu wa kifungu cha 17 (7), katika kazi zake Sheha atawajibika kwa Mkuu wa Wilaya yake.
Ili mtu aweze kuteuliwa kuwa Sheha ni lazima awe na sifa zifuatazo:
(i). awe Mzanzibari;
(ii). awe ni mtu mwenye kuheshimika;
(iii). awe ni mtu mwenye tabia nzuri;
(iv). awe na umri usiopungua miaka 40;
(v). awe amepata elimu ya msingi na anajua kusoma na kuandika kiswahili na/au kiingereza; na
(vi). awe ameishi kwenye shehia hiyo kwa muda usiopungua miaka 15.

Friday, April 22, 2011

Ndoa kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971

KUFUATANA na na sheria ya ndoa ya mwaka 1971, ndoa ni muungano wa hiari kati ya mwanamme na mwanamke unaokusudiwa kudumu kwa muda wa
maisha yao.

Aina za ndoa

Kuna aina mbili za ndoa;
i) ndoa ya mke mmoja, hii ni ndoa ambapo mwanamme ana mke mmoja tu.
ii] ndoa ya wake wengi, hii ni ndoa ambayo
mwanamme ana wake zaidi ya mmoja.
Ndoa itokanayo na dhana ya ndoa; hii ni ndoa ambayo mwanamke na mwanamme wamekaa pamoja ndani ya nyumba kama mke na mme kwa muda wa miaka miwili na kuendelea na wote wakapata hadhi ya kuwa wanandoa.

Vipengele gani vya kuzingatia ili wanaotaka kufunga ndoa wakubaliwe kisheria kufunga ndoa

(a) Ni lazima muungano uwe wa hiari

Mume na mke wawe wameamua kuishi pamoja kwa ridhaa yao wenyewe. Hii inamaanisha kusiwe na kulazimishwa, kuhadaiwa kwa aina yoyote kwani
muungano kama huo utakuwa batili kisheria.
Ni kosa la jinai kushiriki katika shughuli ya ndoa ambayo mmoja wapo au wote wamelazimishwa kufunga ndoa.

(b) Muungano uwe ni kati ya mwanamke na mwanamme

Muungano wa watu wa jinsia moja hata kama ni wa hiari muungano huo hautambuliki kisheria.
Pia mtu huhesabika mwanamke au mwanamme kutokana na
sehemu za siri alizozaliwa nazo na siyo alizozipata baadaye.

Jamii inachukulia kuwa ndoa ni njia pekee
ya kujipanua, upanukaji huku ni kwa kuzaa watoto.

Kwa hali hiyo ili kupata watoto ni lazima ndoa iwe kati ya mwanamme na mwanamke.

(c) Muungano huo uwe unakusudiwa kuwa wa kudumu

Pamoja na kuwa mwanamke na mwanamme wameamua kuishi pamoja kwa hiari yao lakini siyo kwa kutodumu muungano huo hautambuliki kisheria
kama ndoa.

Muungano ni lazima uwe wa kudumu
maisha yote au kama mmoja wao amefariki au kama ndoa imekumbwa na matatizo na mahakama ikaona ni bora kutoa talaka kwa yeyote aliyefika kulalamika.

(d) Wanandoa wasiwe maharimu
Maharimu ni watu walio na mahusiano ya karibu ya damu au kindugu.

Wawili wanaoamua kufunga ndoa wasiwe na uhusiano wa karibu kindugu.

Inakatazwa katika kifungu cha 14 cha Sheria ya ndoa ya mwaka
1971 mtu kuoa au kuolewa na mzazi wake, mtoto au mjukuu wake, kama ni dada yake, mama au shangazi au baba wa mjomba wake, baba au mama wa kambo na mwanaye aliyemfanya kuwa mtoto
wake (adopted child).

(e) Wanandoa wawe wametimiza umri unaokubalika kisheria

Mwanamke na mwanamme wawe wametimiza miaka 18 ili kufunga ndoa.

Hata hivyo mwanamke anaweza kuolewa akiwa na umri wa chini ya miaka18 lakini sio chini ya miaka 15 kama atapata idhini
ambayo hutolewa na baba na kama hayupo ni mama au kama wote wamefariki idhini itatolewa na mlezi wa binti huyo.

Kama wote wamefariki basi hatahitaji idhini.

Kuna wakati katika mazingira fulani
mahakama inaweza kutoa idhini kwa binti kuolewa akiwa na miaka 14 lakini si chini ya hapo ikiwa ataonekana kwa mfano ana mimba.

Pia mwanaume anaweza kuruhusiwa na mahakama kuoa akiwa na umri wa miaka chini ya 18 lakini lakini si chini ya 16
kama ataonyesha kuelewa jukumu lake kama mtu mzima.

Lakini hii ni pale ambapo kuna tatizo kama la kumpa msichana mimba ndipo mahakama inaweza
ikatoa idhini.

Hii inathibitishwa katika ombi la kuoa la Shabiri A. M Virji (1971) HCD no.407 la Mahakama Kuu ya Tanzania, mwombaji alikuwa na miaka 16 lakini
alimpa mimba binti wa miaka 18.

Mahakama katika kuchunguza ombi la mvulana la kuoa ilitoa kibali kwa
sababu wote wawili walipendana sana na wazazi wao hawakuwa na kipingamizi cha wao kuoana.

(f) Kusiwe na ndoa inayoendelea

Kama mwanamke ana ndoa inayoendelea na
inatambulika kisheria haruhusiwi kufunga ndoa nyingine (polyandry).

Kadhalika kama mwanamme
ana ndoa ya mke mmoja au kama ni mwislamu ana wake wanne tayari hataruhusiwa kufunga tena
ndoa.

(g) Kusiwe na kipingamizi

Kama ndoa imezuiwa na Mahakama au halmashauri ya usuluhishi kutokana na uwezo zilizopewa na ndoa ikaendelea kufungwa kabla ya wenye
kupeleka kipingamizi hawajasikilizwa au Mahakama imeshaamua ndoa hiyo isifungwe basi ndoa hiyo
itakuwa ni batili.

(h) Mfungishaji ndoa kutokuwa na mamlaka
Kama wanaofunga ndoa wanajua wazi kuwa
anayewafungisha ndoa hana mamlaka hayo na kwa makusudu wakakubali awafungishe ndoa basi ndoa hiyo itakuwa ni batili.

Mfungishaji ndoa ili kuwa na
mamlaka anapaswa kusajiliwa na Msajili Mkuu wa Ndoa na kupewa leseni ya kufungisha ndoa.

(i) Kutokuwepo kwa wafunga ndoa

Kama ndoa imefungwa bila ya wafunga ndoa wote kuwepo basi ndoa hiyo haitambukuliwa kisheria.

Hata hivyo sheria inaruhusu ndoa kufungwa ikiwa mmoja
wa wafunga ndoa hayupo, kama mfunga ndoa ambaye hayupo amewakilishwa na mtu ambaye alikuwepo wakati mfunga ndoa hayupo, alipotoa ridhaa yake ya kuoa au kuolewa.

(j) Mashahidi wa ndoa

Ili ndoa itambulike kisheria ni lazima ishuhudiwe na mashahidi wasiopungua wawili ambao wanaruhusiwa
kisheria yaani umri wao usipungue miaka 18 na wafahamu kinachosemwa na kutendeka wakati wa kufunga ndoa.

(k) Kuwa katika eda

Eda ni kipindi cha kukaa ndani kinachotolewa kwa mwanamke wa kiislamu aliyeachika katika ndoa au aliyefiwa na mumewe, ili taratibu fulani za kidini
zifanyike.

Kama mwanamke ambaye ndoa ilifungwa kiislamu anaolewa wakati wa kipindi cha eda hakijaisha basi ndoa hiyo itakuwa batili.

Lakini mfaruku hiyo ni pale iwapo mtalikiwa awe anafuata dini ya Kiislamu.

Kama atabadili dini baada ya kufiwa au kupewa talaka masharti ya eda
hayatambana na atakuwa huru kuolewa.

Aina za ufungaji ndoa na taratibu za kufuata

Taarifa ya nia ya kuoa

Kwanza kama mwanamke na mwanamme wanataka kufunga ndoa ni wajibu taarifa ya nia ya kufunga ndoa itolewe kwa mfungishaji ndoa siku 21 kabla ya
siku ya kufunga ndoa.

Taarifa hiyo ionyeshe mambo yafuatayo:-

(i) Majina kamili na umri wa wanaotaka
kuoana.

(ii) Uthibitisho kwamba hakuna kipingamizi
dhidi ya hiyo ndoa wanayotarajia kufunga.

(iii) Majina kamili ya wazazi wao na sehemu
wanakoishi.

(iv) Hadhi ya wafunga ndoa, yaani kama ni
mwanamke ifahamike kama hajaolewa,
ametalakiwa au ni mjane na mwanamme
pia anapaswa kama hajaoa, au ana mke au/wake wengine (hii ni kwa ndoa za
kiserikali na kiislamuu) au kama ametaliki.

(v)Kama muolewaji ana umri chini ya miaka 18, jina la mtu aliyetoa idhini ya yeye
kuolewa kama yupo ionyeshwe.

(vi) Kama ni ndoa ya kiserikali au kiislamuu
hapana budi kueleza kama ndoa ni ya wake
wengi au inatazamiwa kuwa ya wake wengi,
majina ya wake waliopo yatajwe.

Pia katika fungu hili kama mtu anataka ndoa iwe ya mke mmoja anapaswa kueleza.

Baada ya taarifa yenye maelezo haya kufikishwa kwa mfungishaji ndoa yeye anawajibika kutangaza hii nia ya kufunga ndoa.

Sababu ya kufanya hivyo ni ili kama kuna mwenye kipinganizi na ndoa hiyo atoe taarifa.

Matangazo haya hutolewa kama ndoa inatarajiwa kufungwa kidini, sehemu za ibada.

Kama ni ndoa ya kiserikali tangazo litabandikwa nje ya ofisi ya msajili wa Ndoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya.

Vipingamizi vya ndoa viko vya aina
mbili, cha kwanza ni kile cha kisheria yaani
kama ndoa itakayofungwa itakuwa batili.

Kipingamizi cha pili ni kama muoaji ana mke au wake wengine tayari, hivyo mke au wake wanaweza kutoa kipingamizi kama uwezo wa muoaji kifedha ni mdogo kiasi kwamba kuongeza mke mwingine kutazidisha shida.

Mfungishaji ndoa anapopokea taarifa ya kupinga ndoa isifungwe, ataipeleka taarifa hiyo kwenye Baraza la Usuluhishi la Ndoa.

Huko aliyewekewa kipingamizi na aliyeweka wataitwa na kila mmoja
atajieleza.

Baada ya kusikiliza pande zote Baraza
lina uwezo wa kuamua ndoa hiyo ifungwe au isifungwe na mfungishaji ndoa atafuata uamuzi wa Baraza.

Kama mtu atatoa kipingamizi cha uongo na
ikithibitika hivyo, adhabu yake anaweza kufungwa kifungo kisichozidi miaka mitatu.

Baada ya kipengele hiki kutimizwa ndoa inaweza kufungwa.

Aina za ndoa

Kama tulivyosema awali kuna aina mbili za ndoa.

(a) Ndoa ya mke mmoja

Huu ni muungano unaoruhusu mwanamme kuoa si zaidi ya mke mmoja, mfano wa aina hii ya ndoa ni ndoa ya Kikiristo.

(b) Ndoa ya zaidi ya mke mmoja

Huu ni muungano unaoruhusu mwanamme kuoa mke zaidi ya mmoja, mfano wa aina hii ya ndoa ni ndoa za Kiislamu na ndoa za kimila.

Sheria ya ndoa inatambua aina tatu za ufungaji wa ndoa yaani kiserikali, kidini na kimila.

Ndoa hizo zaweza kufungwa kwa kufuata taratibu za kidini au za kiserikali.

Utaratibu huo utafuata au kuzingatia kama wanandoa ni waumini wa dhehebu
fulani au la.

(a) Ndoa ya kidini

Ndoa hii hufungwa kwa mujibu wa taratibu ya dini husika hivyo ni lazima masharti yote yatimizwe kisheria na taarifa ya nia ya kufunga ndoa itolewe na ndoa
ifungiwe mahali pa wazi panapokubalika kisheria na mfungishaji awe na mamlaka hayo kisheria.

(b) Ndoa ya kiserikali

Ndoa hii hufungwa mbele ya Mkuu wa Wilaya ambaye ndiye Msajili wa Ndoa.

Ndoa itafungwa katika ofisi ya Msajili au mahali pengine popote palipotajwa
katika leseni yake ya kufungisha ndoa.

(c ) Ndoa ya kimila

Ndoa inaweza kufungwa kimila iwapo mmoja wa wafunga ndoa au wote wawili wanafuata sheria za
mila za kabila fulani ambapo mwandishi wa ndoa za kimila ni Katibu Tarafa.

Ndoa ya kimila hufungishwa na
mtu anayetambulika kimila kuwa ana uwezo huo.

Ni muhimu sana Katibu Tarafa kuhudhuria kwenye ufungishaji huo wa ndoa kwani ndiye atakayehusika na kuleta vyeti vya ndoa kutoka kwa msajili.

Ufungaji ndoa nje ya nchi

Kifungu cha 8 cha sheria kinampa mamlaka Waziri wa Sheria kuteua baadhi ya maofisa ubalozi kuwa wasajili wa ndoa.

Ni lazima msajili aridhike kuwa masharti yote yametimizwa ndipo afungishe ndoa.

Kuna masharti ya nyongeza kama angalau mmoja wa wafunga ndoa awe ni Mtanzania. Pia kama mmoja wa wafunga ndoa si Mtanzania ni lazima Msajili aridhike kuwa ndoa inayokusudiwa kufungwa
itatambulika kisheria katika nchi ambayo huyo mmoja wa wafunga ndoa ni mkazi.

Utaratibu unaotumika kufungisha ndoa hizi ni sawa na ule unaotumika
katika kufungisha ndoa za kiserikali.

Dhana ya kuchukulia ndoa

Kuna dhana inayokanushika (rebuttable
presumption) kuwa mwanamme na mwanamke wakiishi pamoja kwa miaka miwili au zaidi huchukuliwa kuwa ni mke na mume mbele ya sheria
japokuwa hawakuwahi kufunga ndoa. Dhana hii imeelezwa katika kifungu cha 160 cha Sheria ya Ndoa.

li dhana hii iwepo ni lazima yafuatayo yathibitishwe.

(i) Lazima ithibitike kwamba mwanamke na mwanamme wameishi pamoja kwa muda wa miaka miwili au zaidi kwa mfululizo.

(ii) Lazima pia ithibitike kuwa umma
unaowazunguka unawachukulia na
kuwapa heshima kama mke na mume.

(iii) Lazima ithibitishwe kuwa watu hao
walikuwa na uwezo wa kuwa mke na mume
wakati walipoanza kuishi pamoja kama
umri ulikubalika kisheria.

(iv) Ni lazima pia ithibitishwe kuwa kati ya hao wawili au wote hakuna aliye na ndoa
inayoendelea.

Ndoa batili na sababu zinazoweza kuifanya ndoa kuwa batili

Ndoa batili ni ndoa ambayo itachukuliwa kisheria kuwa ni ndoa halali hadi hapo amri ya kuivunja itakapotolewa.

Ndoa batili ni halali kama ndoa
nyingine isipokuwa ina kasoro fulani.

Wanandoa katika ndoa hiyo wana haki na wajibu sawa kama ilivyo katika ndoa nyingine zisizo na kasoro.

Kadhalika watoto waliozaliwa katika ndoa ya namna hii ni halali
na wana haki zote kisheria.

Ni vitu gani vinavyofanya ndoa kuwa batili?

1. Maradhi ya zinaa

Kama wakati wa kufunga ndoa mmoja wa wafunga ndoa alikuwa na maradhi ya zinaa na yule asiye na ugonjwa kama wakati wa kufunga ndoa alikuwa hajui lolote anaweza kulalamika mahakamani na
ndoa ikavunjwa.

2. Kukataa makusudi kutimiza ndoa

Kama baada ya kufunga ndoa mmoja wa wafunga ndoa atakataa kuitimiliza ndoa anayekataliwa ana haki ya kuiomba mahakama kuvunja ndoa
hiyo.

Maingiliano yanayotambulika kisheria ni yale yanayofanyika siku ya ndoa na kuendelea na siyo kabla ya ndoa.

Kukataa kuitimia ndoa kunakuwa
sababu ya kubatilisha ndoa ikiwa mwenye kukataa hana sababu yoyote ya msingi na mwenye kukataliwa ametumia kila mbinu kumshawishi aliyekataa lakini
ikashindikana kufanya tendo la ndoa.

3. Mimba ya mwanamme mwengine

Kama wakati wa kufunga ndoa mke atathibitika ana mimba aliyopata kwa mwanamme mwingine, mume
anaweza kuiomba mahakama ivunje ndoa hiyo.

Kama itathibitika kuwa mume alijua hivyo hali wakati wa kufunga ndoa, lalamiko lake halitasikilizwa.

4. Wazimu au kifafa cha kipindi

Mmoja wa wafunga ndoa kama ana wazimu au kifafa cha kurudia rudia na mwenzake alikuwa hajui hilo hali wakati wa kufunga ndoa, atakuwa na haki ya kuiomba mahakama kuivunja ndoa hiyo.

Ieleweke kuwa ugonjwa ni lazima uwe unarudia rudia na siyo mtu awe aliugua na akapona.

5. Kushindwa kutimiza ndoa

Kama mmoja wa wafunga ndoa atashindwa kuitimiliza ndoa basi ndoa hiyo inaweza kubatilishwa.

Kwa mwanamme kama anashindwa kuitimiliza ndoa kwa sababu ya kukosa nguvu za kiume basi ana haki ya
kuiomba mahakama kuibatilisha ndoa.

Ili kukosa nguvu za kiume kuwe sababu ya kubatilisha ndoa ni lazima ithibitike kuwa hali hiyo ilitokea kabla au wakati
wa kufunga ndoa na siyo baada ya kufunga ndoa wakati kitendo cha kuitimiliza ndoa kilishafanyika.

Ili ndoa iweze kubatilika ni lazima kukosa nguvu huko kuthibitishwe na daktari kuwa hakuponi au kunapona lakini mwanamme hataki matibabu.

Mwanamke anaweza kuwa na maumbile ambayo yanaweza kufanya ndoa ishindwe kutimilizika.

Ikithibitika hali hiyo lakini mwanamke hataki tiba mwanamme
anaweza kuomba mahakamani ndoa kubatilishwa.

Ili mahakama iweze kusikiliza shauri la kuomba kubatilisha ndoa ni lazima shauri hilo lipelekwe haraka.

Kama shauri litakwenda mahakamani baada ya mwaka mmoja tangu tarehe ya ndoa Mahakama haitalipokea.

Pia ni lazima ithibitike kuwa mlalamikaji
alikuwa hajui kasoro hiyo wakati wa kufunga ndoa na baada ya kuigundua kasoro hiyo hajawahi kuingiliana
na mwenzie mwenye kasoro hiyo.

Ndoa batili huvunjwa na mahakama pekee baada ya kupokea malalamiko toka kwa mmoja wa wanandoa.

Kama hakutakuwa na malalamiko yatakayopelekwa mahakamani na anayedhurika na kasoro hizo, ndoa
hiyo itadumu ama labda mmoja afariki au kama kuna talaka itatolewa na mahakama.

Watu waliooana wana uhuru wa kugeuza ndoa yao kuwa ya mke mmoja au ya wake wengi pale wanapofuata taratibu zinazokubalika kisheria.

Kabla ya kufanya uamuzi wa kugeuza ndoa ni hapanabudi wanandoa wakubaliane kuhusu uamuzi huo.

Kitendo cha kugeuza ndoa hufanywa mbele ya Hakimu wa Wilaya au Jaji ambapo wanandoa watatoa tamko la maandishi lenye saini zao na Hakimu au Jaji
aliyeshuhudia naye hutia sahihi yake.

Katika kugeuza ndoa, ndoa ya kiserikali ya kienyeji au ya Kiislamu inaweza kugeuzwa kuwa ya mke mmoja kama kabla ya kugeuza hizi zinaweza kugeuzwa
kuwa ya wake wengi.

Ikumbukwe kuwa kubadilisha dini pekee hakubadilishi hadhi ya ndoa.

Vilevile ndoa ya kikristo haiweza
kugeuzwa kuwa ya wake wengi wala ndoa ya wake wengi inayodumu kuwa ya mke mmoja.
Talaka na taratibu zake

Talaka ni ruhusa au amri ya mahakama ya kisheria ambayo mume au mke hupewa wakati anapomwacha mwenzake.

Chombo chenye mamlaka ya kutoa talaka ni
mahakama tu.

Mahakama hiyo itatoa talaka kwa
ndoa ambayo imedumu kwa muda wa miaka miwili au zaidi.

Mahakama inaweza kutoa talaka kwa ndoa
ambayo haijafikisha muda huo endapo mlalalmikaji atatoa sababu za msingi mahakamani.

Kutengana

Kutengana si talaka,kutengana maana yake ni hali ambayo mke na mume hukaa mbalimbali.

Kukaa mbalimbali au kutengana kwaweza kuwa kwa mapatano kati ya wanandoa hao au kutengana kwaweza kuwa kwa amri ya mahakama.

Mahakama itatoa amri hiyo endapo mmoja wao atapeleka maombi mahakamani.

Faida ya kutengana wote au mmoja wao waweza au aweza kutambua makosa na baadaye kukata shauri kurudiana au kuishi tena.

Kutengana kwa mapatano, ni kutengana kwa hiari yao wenyewe bila shuruti, mapatano hayo yaweza kuwa ya maandishi au ya mdomo.

Mambo kadha yaweza kuzingatiwa wakati wa makubaliano kama; heshima kwa kila mmoja, matumizi au matunzo,watoto kama wapo watakaa na nani, mali ya pamoja je itatunzwa namna gani na kutobughudhiana.

Kutengana kwa amri ya mahakama, hii ni hali ya mume na mke kutengana kwa amri ya mahakama na mahakama imeridhika kuwa ndoa imevunjika.

Ushahidi wa kuwa ndoa imevunjika ni ushahidi ambao unaweza kutolewa mbele ya mahakama kunapokuwepo na maombi au shauri la talaka.

Sababu za kutoa talaka mahakamani

Kabla ya kupeleka shauri au maombi mahakamani ya talaka, mwanandoa husika hana budi kufuata au kuzingatia hatua zifuatazo;

a) kufungua au kupeleka malalamiko
kwenye Baraza la Usuluhishi la Ndoa kwa mfano Bakwata, kanisani,Ustawi wa Jamii au Baraza la Kata.

b) Baraza litasikiliza, na endapo litashindwa mapatano au muafaka kati ya wanandoa hao, basi baraza litatoa cheti ambacho kitaeleza kuwa limeshindwa kusuluhisha mgogoro wa ndoa na kuomba
mahakama kuendelea kutoa talaka.

c) Baada ya mwanadoa mmoja kupata cheti
hicho basi atatakiwa atayarishe madai ya
talaka akionyesha kuwa kulikuwa na ;-
ndoa halali, kuna mgogoro kati yao,
watoto, mali walizochuma wakati wa ndoa yao,.

Muombaji huyo ataiomba mahakama hiyo itoe amri ya talaka, mgawanyo wa mali zilizochumwa kwa nguvu za amoja,mamlaka ya kukaa na watoto na matunzo yao, gharama za madai au shauri.

Ili mahakama itoe talaka sababu kadha huangaliwa na mahakama.

Sababu hizo ni mambo ambayo
yatakayofanya ndoa ionekane kuwa imevunjika kiasi kwamba haiwezi kurekebishika tena, mambo hayo ni
kama ifuatavyo;

a) Ugoni; hii ni zinaa ambayo hufanywa na
mwanamme na mwanamke ambao hawajaoana.

Hii hutokea ambapo mwanamme ana mke wake au mwanamke ana mume wake, hivyo mmoja wapo anamwacha mke/mume na kufanya zinaa na mtu mwingine.

b) Ukatili; ukatili ni kuumiza nafsi nyingine, kuharibu mwili au kuwa na hofu ya kuumizwa.
c) Kulawiti; kulawiti ni kumwingilia mtu kinyume na maumbile,

d) Kichaa; ni kutokuwa na akili timamu, na hali hii lazima iwe imethibitishwa na madaktari bingwa wa akili.

e) Kuzembea wajibu kwa makusudi; haya ni majukumu ya mume, majukumu hayo ni kama haya; kumtunza mke kwa kumpa chakula, malazi na mavazi.

f) Uasi; ni hali ya mke au mume kuhama nyumba ya ndoa na kwenda kuishi mahala pengine bila sababu yoyote ya msingi,

g) Kutengana; kukaa mbalimbali kwa mume na mke kwa muda wa miaka isiyo pungua mitatu, kutengana kwao ni sababu tosha ya talaka.

h) Dhana ya kifo; hii ni hali ambayo mmoja wa wana ndoa amekufa, na hii hutokea iwapo mojawapo hataonekana / ametoroka kwa muda mrefu, kama miaka 5, hapo mahakama hutoa tangazo kuwa
fulani amekufa.

i) Kifungo; hii ni hali ambayo mume au mke ametenda kosa la jinai na ametiwa hatiani na mahakama imemfunga miaka 5 au maisha basi mahakama
inaweza kutoa talaka kwa mwombaji.

j) Tofauti za imani za kidini, endapo mwanandoa mmoja atabadili dini basi ni sababu tosha ya kuomba
mahakama ivunje ndoa na kutoa talaka.

Haki na wajibu katika ndoa

Baada ya kufunga ndoa na ikaonekana haina kasoro yoyote, mke ana haki mbalimbali kisheria anazostahili
kuzipata.

Haki hizi ni kama; Matunzo; mke au wake wana haki ya kutunzwa na mume wao kwa kuwapatia mahitaji muhimu kama
chakula, malazi, mavazi, matibabu, n.k kulingana na uwezo alionao mume.

-Kumiliki mali; mke ana haki ya kumiliki mali aliyoipata kabla na baada ya ndoa kama aliipata kwa fedha yake mwenyewe.

-Mke ana haki ya kuingia mikataba, kushitaki na kushitakiwa.
- Makubaliano yaweza kufanywa na wanandoa hiyo jinsi ya kumiliki
mali iliyopatikana kabla ya ndoa yao jinsi gani waimiliki. Kwa mali iliyopatikana wakati wa ndoa, mali hiyo ni mali ya wanandoa wote, kwa sababu
imepatikana kwa mchango wa nguvu za pamoja.

Hii haijalishi kuwa mmoja wa wanandoa (mke) hachangii pesa tasilimu au anakaa nyumbani na kufanya shughuli za nyumbani tu.

Kufanya shughuli za nyumbani ni mchango mkubwa na ameokoa fedha
nyingi.

Umiliki wa mali kwa wanandoa haujalishi
kuwa mmoja wapo amemiliki mali hiyo kwa jina lake au la.

Haki ya kukopa kwa dhamana ya mume; jukumu la kutunza mke na watoto ni jukumu la mume au
baba.

Kwa msingi huo, endapo baba amesafiri,
au ametoroka na baadaye matatizo yakajitokeza yanayohitaji fedha, basi mke ana haki ya kukopa fedha kwa jina la mume au kuweka rehani mali yamumewe.

- Haki ya kuishi katika nyumba ya ndoa;
Nyumba ya ndoa ni nyumba ambayo mke na mume wanaishi wakati wa ndoa. Hata kama wanandoa wana nyumba nyingi, basi wanayoishi au kutumia
kama makazi ndiyo nyumba ya wanandoa.

Nyumba hii haiwezi kuuzwa, kuweka rehani au kuchukuliwa na mtu mwingine kama zawadi bila ya makubaliano ya wanandoa wote.(bila ridhaa ya wanandoa).

Mwanandoa ana haki ya kuishi kwenye nyumba hiyo mpaka amri ya mahakama ya kuvunja ndoa, au kutengana itakapotolewa.

Talaka kisheria
Neno talaka linaweza kuwa mojawapo ya maneno yaliyozoeleka midomoni au masikioni mwa watu wengi katika ulimwengu wa sasa.
Kwa lugha nyepesi, talaka ni kitendo cha wanandoa kuachana na mahusiano ya kindoa yaliyokuwa baina yao.
Lakini kisheria, ingawa maana ya talaka inaakisiwa na maana hii ya Kiswahili, lakini katika maana ya sheria kuna mambo mengine zaidi ya kuzingatia.
Tafsiri ya sheria ya ndoa ya Tanzania, sura ya 29 ya marekebisho ya sheria ya mwaka 2002, talaka ni kitendo cha mahakama yenye mamlaka katika shauri linalohusika, kutoa tamko la kuivunja ndoa iliyokuwapo,kwa sababu mbalimbali.
Hivyo, tukiangalia kwa mtazamo wa kihistoria, ndoa kwa mujibu wa sheria ya Kiingereza (common law) ambayo imeakisiwa sana na sheria ya ndoa ya Tanzania, ilikuwa haitambui sababu ya aina yeyote katika kuivunja ndoa kwa msingi wa talaka.
Lakini baada ya miaka mingi kupita, sheria ya talaka ilianza kutumika nchini Uingereza baada ya sababu kadhaa za kisheria za kuvunja ndoa kwa talaka kuanzishwa.
Sheria ya Talaka (The Divorce Act) ya mwaka 1969 ilianzishwa nchini Uingereza kufuatia ripoti ya askofu Kent wa nchini humo.
Mwaka mmoja baadaye yaani mwaka 1969 serikali ya Tanzania kupitia tamko la serikali (Government Notice) namba 1 ya mwaka huo, iliyojulikana kama White Paper ilichukua msimamo na mtazamo huu wa sheria ya Kiingereza juu ya talaka.
Hadi mwaka 1971 tulipochukua msimamo huu wa sheria ya Uingereza juu ya talaka, mabadiliko makubwa ya kimsingi ya sheria juu ya talaka yalitokea katika sheria yetu hapa nchini nayo ni pamoja na kuwa na sababu moja tu inayoweza kuifanya ndoa kuvunjwa na mahakama kwa tamko la talaka, sababu hiyo ni kuwa mahakama itakapothibitisha kwamba ndoa hiyo imevunjika kabisa na haiwezi kurekebishika kutokana na kasoro zisizo weza kurekebishika.
Hivyo, sheria ya Tanzania katika hili nayo ikachukua sababu moja inayoweza kuifanya ndoa kuvunjwa na talaka.
Hata hivyo, wakati tunaangalia sheria hii, tunatakiwa kujua kwamba sababu moja ya kuivunja ndoa kwa talaka ipo Tanzania bara pekee.
Baadhi ya watu wanadhani sababu za kuvunja ndoa ni zile zinazoelezewa na sheria hii kama hali au mazingira ya kuthibitisha kwamba ndoa hiyo ina tofauti zisizorekebishika.
Sababu hizo ni pamoja na uzinifu nje ya ndoa, ukatili pamoja na kumkimbia/kumtelekeza mwanandoa mwezako.
Uzinifu ni mojawapo ya sababu zinazoipa mahakama mamlaka kisheria kuivunja ndoa yoyote.
Hata hivyo, unatakiwa kujua uzinifu una maana nyingi kutegemea na eneo husika.
Kimsingi uzinifu ni kitendo cha mwanandoa mmoja kufanya ngono nje ya mahusiano yake ya ndoa iliyo halalishwa.
Hapa katika kuondokana na wasiawasi wa kuweza kushindwa kuthibitisha uzinifu, sheria imetoa dhana kwamba pale tu itakapokutwa mume na mke wamelala pamoja na wako watupu, basi dhana hapa ni kwamba wametoka au wanataka kufanya ngono.
Dhana hii kama ilivyoanzishwa na mahakama katika shauri la Denise dhidi ya Denise, Jaji Single anasisitiza kwamba dhana hii ni ngumu kuipinga isipokuwa kama itathibitika kwamba mwanaume aliyekutwa ni hanithi au mwanamke huyo ni bikira.
Na uthibitisho wa uzinifu nje ya ndoa ni kama uthibitisho wa katika kesi ya jinai ambapo anayelalamika anatakiwa kuithibitishia mahakama pasi na shaka kwamba uzinifu umetokea.
Kwa upande wa Uingereza, kama itathibitika kwamba kulikuwa na uzinifu na kwamba mtoto alizaliwa nje ya ndoa, pia atahesabika ni mtoto haramu na hivyo kukosa haki zake zote kwa mzazi wake wa pili.
Hata hivyo, mara nyingi uzinifu unaweza kuthibitishwa na ushahidi wa mazingira kama vile mmoja wa wanandoa kuwa na ugonjwa wa zinaa na kadhalika.
Kifungu cha 170(2) cha sheria ya ndoa ya Tanzania, kinatoa maelekezo juu ya ushahidi wa aina hii.
Hata hivyo, uzinifu si lazima uwe sababu ya mahakama kutoa talaka. Mahakama kwa kuzingatia mazingira ya kesi husika inaweza kuamuru mtu aliyefanya uzinifu na mmoja wa wanandoa kumlipa fidia muathirika wa uzinifu huo.
Ukatili pia ni sababu mojawapo ya sababu zinazoweza kuithibitishia mahakama kwamba ndoa hii ina kasoro zisizoweza kurekebishika.

Kuharamisha, kubatilisha ndoa katika Sheria ya Ndoa

NENO kuharamisha ni la kawaida katika lugha ya Kiswahili ambalo linalotokana na neno ‘haramu’ likimaanisha kitu kisichofaa, kwa maana iliyo nyepesi.
Aidha kuharamisha ndoa kisheria ni kitendo cha mahakama kutoa tamko kwamba ndoa ambayo iliyodhaniwa kuwa imefungwa haikufungwa wala haikuwapo.
Hapa tunatakiwa tujue mantiki ya kitendo hiki ni kuharamisha (nullify) ndoa ambayo ilidhaniwa ni halali wakati wa kufungwa, lakini kumbe katika jicho la sheria ndoa hiyo “haipo na wala haikuwahi kuwapo”.
Hii siyo talaka kama ambavyo watu wengine wanaweza kufikiri. Somo la talaka tutalizungumzia baadae katika makala nyingine.
Kama ambavyo nadharia nyingi za sheria zetu zimetoka katika sheria za mahakama za nchini Uingereza, yaani Common law, nadharia hii imetoka huko huko, wakati wa mageuzi baada ya kuanguka kwa dola ya utawala wa kifalme wa Kirumi huko Ulaya.
Wakati wa utawala wa kirumi huko Ulaya, sheria za Kanisa Katoliki zilikuwa zinatumika kwa kiwango kikubwa, imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki ndoa ni Sakramenti iliyoanzishwa na Mwenyezi Mungu.
Hii ilikuwa na maana kuwa ndoa ni takatifu hivyo talaka ni kitu ambacho hakitambuliki katika sheria za Kanisa, kusisitiza maneno ya bwana Yesu katika Injili ya Marko 10:7-8 kwamba mwanaume na mwanamke wakiungana wanakuwa mwili mmoja na kwamba alichokiunganisha Mungu mwanadamu yeyote asikitenganishe.
Kwa mantiki hiyo, njia pekee ya watu kutoka ndani ya ndoa wakati huo ilikuwa ni kuiharamisha na si talaka, kwani ilikuwa haitambuliki kama tulivyoona hapo awali. Baada ya kuanguka kwa dola ya Rumi huko Ulaya, tawala za kifalme zikawa maarufu sehemu nyingi huko Ulaya na kusababisha sheria za kanisa (Canon law) kupotea na kwa upande wa Uingereza, sheria za mahakama za Uingereza yaani Common law zikashika kasi.
Hivyo basi athari ya sheria hizi za mahakama za Uingereza ilikuwa ni pamoja na kuleta mafundisho mengine ikiwemo kuanzisha upya talaka.
Kwa Tanzania, vifungu vya 39 na 49 vya Sheria ya Ndoa, 1971; vinaelezea njia mbili kuu za kuharamisha ndoa. Njia hizi ni zile ambazo ikithibitika mahakamani, basi mahakama itatoa tamko la kuharamisha ndoa.
Njia hizi ni pamoja na ndoa haramu (void marriage) na ndoa isiyo haramu lakini pia si halali kwa kuwa imekosa mahitaji kadhaa ya kisheria yaani ndoa batili ( voidable marriage).
Kwa ndoa haramu, hii ni ndoa ambayo tangu mwanzo ilikuwa ni haramu katika jicho la sheria; wakati aina ya pili ya ndoa isiyo haramu ila imekosa kutimiza masharti kadhaa ya kisheria kuifanya iwe halali na hivyo kuifanya batili.
Kwa mfano kwa mwanamme asieweza kufanya tendo la ndoa na mkewe, ndoa yake itakuwa batili kama mkewe atakwenda mahakamani kuomba ndoa yake ibatilishwe kwa kuwa mumewe hawezi kufanya tendo hilo ambalo ni hitaji la kisheria ili ndoa iwe halali; lakini kama mwanamke huyo atavumilia hali hiyo, ndoa yao itakuwa ni halali.
Hivyo basi, kwa mujibu wa kifungu cha 39 na 49 vya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, kuna sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha ndoa isiwe halali, kwa sababu hizo mume au mke anaweza kuomba mahakama itoe tamko la kubatilisha ndoa yake. Sababu hizi ni kama zifuatavyo;
Kwanza, kwa wanandoa kushindwa kufanya tendo la ndoa wakati wameoana, kwa mujibu wa kifungu cha 39(e) cha Sheria hii, pindi mwanandoa yeyote (mwanamme au mwanamke) wakati wameshafunga ndoa na mwenzake atashindwa kufanya tendo la ndoa hiyo itakuwa sababu kwa mmojawapo kuomba tamko la kubatilisha ndoa hiyo.
Huu pia ni uamuzi uliotolewa katika shauri la Dralge dhidi ya Dralge , (1947)1 All.ER 29), la nchini Uingereza,ambapo mahakama ilitafsiri kimantiki kwamba tendo la ndoa ndilo haswa linalomaanishwa katika kile ambacho kifungu cha 39 cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 inamaanisha.

Monday, April 18, 2011

Tupambane na wanaowapa ujauzito watu wenye ulemavu kisha wakawatelekeza

MATUKIO ya wanawake walemavu kupewa ujauzito na kisha kutelekezwa yanaongezeka kila uchao katika jamii yetu.
Tumeyasikia mara kadhaa na mengine yamekuwa yakiwakumba ndugu zetu wa karibu katika nyumba tunazoishi.
Watu wenye ulemavu wamekuwa wakirubuniwa na wanaume wenye tamaa ya ngono na baada ya kupata wanachohitaji wanawakimbia na kuwaacha katika mateso makubwa ya kulea ujauzito.
Ndio ni haki na ni wajibu kwa mlemavu kuwa na familia yake, lakini siyo kwa kwa kupewa ujauzito vichochoroni na kisha kutelekezwa na kuachwa katika mazingira magumu ya maisha.
Walemavu wengi hawana elimu, hawana ajira na mazingira yao ya kujipatia kipato ni magumu mno kiasi cha kuwafanya wakati mwengine kuishi ama kwa msaada wa ndugu zao au kujitahidi kufanya kazi hata zile ngumu huku wengine wakigeuka kuwa omba omba.
Bila shaka hakuna atakaebisha kuwa watu wenye ulemavu ni miongoni mwa omba omba katika mitaa yetu mengi, hii yote ni kwa sababu tumewasahau.
Wanapoongezewa tatizo jingine zito kama la ujauzito na kisha kutelekezwa ni kuwazidishia machungu kiuchumi na kisaikolojia wao pamoja na familia zao.
Ni ukatili na ukosefu wa imani kwa binadamu kuwa na tamaa kiasi cha kumbebesha ujauzito mwanamke mwenye ulemavu na kisha kumtoroka au kuukana ujauzito.
Tabia hii sio tu inapigiwa kelele kwa watu wenye uleamvu, lakini pia haipendezi kufanyiwa watu wengine wasiokuwa na ulemavu, lakini linapotokea kwa watu wenye ulemavu huwa ni machungu zaidi kutokana na maumbile yao.
Kitendo cha kufanya mapenzi kinapaswa kuwa shirikishi kwa maana ya kuwahusu moja kwa moja wazazi na hivyo ridhaa ya kufanya tendo hilo lazima ipatikane kwa wote na pale inapotokea mama akapata ujauzito ni wajibu wa baba nae kuwajibika hadi ujauzito huo utakapozaliwa.
Hivyo inapotokea mmoja kuachiwa jukumu hilo pekee linakuwa ni tatizo si kwake tu, hata kwa kiumbe atakayezaliwa kwani atakuwa amekosa matunzo ya baba.
Sasa jukumu hilo linapoachwa kwa mwanamke mwenye ulemavu hali inakuwa ni ya mashaka sana kwa sababu uwezo wake wa kumlea mtoto huyu ni mdogo na hasa pale atakapokosa msaada wa baba na mama kama wataamua kumtenga.
Huu ni ukatili mkubwa kwa kuwa kitendo hicho kina matokeo mabaya kwao kwa sababu hawana uwezo wa kujitetea wasifanyiwe hivyo, hawana uwezo wa kiuchumi wa kumudu ulezi wa mimba wala mtoto atakayezaliwa na isitoshe hawana uhakika wa mlo wao wa siku na ndio maana nikasema wanapoachiwa jukumu hilo maisha yao yanakuwa ya mashaka makubwa.
Ni wanaume wachache ambao huwa na mapenzi ya dhati kiasi cha kuoa au kulea mimba wanazowapa wanawake wenye ulemavu, lakini wanahesabika kwa sababu wengi wanaamini kufunga ndoa na mlemavu ni mzigo.
Asilimia kubwa huwarubuni na kuwapa mimba na kisha kutokomea; tumeshawahi kusikia taarifa za hata wagonjwa wa akili kupewa ujauzito na kisha kutelekezwa.
Nilishawahi kuzungumzia adha nyingine wanazokumbana nazo wenzetu walio na ulemavu, kwa kiwango kikubwa wamekosa mazingira rafiki ya miundombinu kama majengo, usafiri na elimu.
Tunapozungumzia kutelekezwa kwa walemavu, waathirika wakubwa ni wanawake kwa sababu ndio walioko katika tabaka la kunyanyaswa na kukosa haki zao za msingi.
Kukataliwa, kupewa ujauzito, kubakwa, kutelekezwa ,kukoseshwa elimu na ajira ni madhila machache kati ya mengi yayowakumba watu wenye ulemavu.
Hizi ni changamoto kubwa ambazo kama hatutakubali kuzifanyika kazi, azma yetu ya kupambana na umaskini na unyanyasaji wa kijinsia haitafanikiwa.
Kwa upande wetu watu wenye ulemavu, wawe tayari kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola, kuwafichua wale wenye tabia ya kuwapa ujauzito walemavu, badala ya kuendelea na tabia ya kuwastiri kwani kuwaficha wahalifu ni sawa na kuchangia kufanya uhalifu.
Aidha Jumuiya za watu wenye ulemavu kama UWZ, zinapaswa kuandaa mikakati endelevu ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wanachama wenu kuweza kujiamini na kuhakikisha hawarubuniwi na wapenda ngono kiasi cha kubebeshwa ujauzito na baadae kutelekezwa.

Kuondolewa muswada wa katiba ni ushindi wa kwanza kwa Watanzania

WIKI iliyopita serikali ya Tanzania ilikubali kuuondoa muswada wa katiba baada ya Kamati ya Sheria na Katiba ya Bunge kuomba marekebisho kadhaa ikiwemo kuletwa kwa lugha ya Kiswahili, na kutangazwa kwenye magazeti ili uwafikie Watanzania wengi popote walipo.
Kuondolewa kwa muswada huu, ni ushindi mkubwa wa kwanza kwa wananchi, ambao tayari walishaanza kampeni mbali mbali za kuupinga kiasi cha kufikia hatua ya kuchanwa na kuchomwa moto.
Ni dhahiri kwamba muswada huu ulikuwa ukijadiliwa na Wabunge bila ya wananchi kushirikishwa, kwani ni kundi dogo sana la wananchi ndio lililopata fursa ya kuuona au kuusoma.
Kwa mara ya kwanza, tuliushuhudia wakati Kamati ya Sheria na Katiba ya Bunge, ilipofanya mikutano yake miwili hapa Zanzibar tena kwa muda mfupi sana, lakini kundi kubwa lililo nyuma yetu, lilikuwa likisikia tu.
Hatua ya Kamati ya Sheria na Katiba, kuomba muda zaidi ni ishara kwamba imekisikia kilio cha wananchi walio wengi, kwamba muswada haujawafikia na hivyo Bunge lisingepaswa kuujadili.
Kwa mfano katika maeneo mengi ya Tanzania, hasa Unguja na Pemba wananchi wengi walikuwa hawafahamu kinachoendelea; ndio walikuwa wakifuatilia vyombo vya habari lakini maudhui ya muswada huu walikuwa hawayaelewi kutokana na kikwazo cha lugha.
Lugha iliyotumika kwenye muswada huo ni Kingereza, wakati wananchi waliopelekewa wengi wao hawafahamu kabisa lugha ya kingereza, hivyo wasingeweza kujadili kitu wasiochokifahamu.
Kuvishirikisha vyombo vya habari kutangaza muswada huu ndio hatua pekee ya kutafuta mawazo ya wananchi ambao ndio wanaoguswa na mabadiliko ya katiba.
Ingekuwa dhambi kubwa kwa Wabunge ambao wamechanguliwa na wananchi kujadili muswada ambao hauna baraka zao na kitendo hichi kingekuwa cha usaliti mkubwa kwa wananchi.
Mbali na marekebisho hayo, Tume ya Katiba na Sheria, pia inapaswa kuyazingatia yote yale iliyokusanya katika kipindi kifupi kutoka kwa wananchi, hasa yake kutoka upande wa Zanzibar.
Tunataka kuitanabahisha Tume kuwa hakuna cha kubeza katika michango ile, vyenginevyo yanaweza kutia doa kubwa yatakapopuuzwa kiasi cha kuwepo kampeni ya ‘Yes’ na ‘No’, kama ilivyotokea Kenya.
Aidha, mtakapopeleka muswada huu kwenye vyombo vya habari kwa ajili ya kuchapwa msiwasahau watu wenye ulemavu, hasa watu wasioona kwa sababu na wao kama raia wa Tanzania wana haki ya kutoa mchango kama yalivyo makubndi mengine.

Sheria inamtoa hatiani kwa kosa la jinai mtoto wa kiume aliye chini ya miaka 12

KWA kipindi kirefu kati ya miaka ya 1996 hadi mwanzoni mwa mwaka 1998, Tanzania kama nchi ilishuhudia kuongezeka kwa kiasi kikubwa makosa ya jinai yanayohusiana na ngono.

Kwa wengi waliokuwa wakifuatilia vyombo vya habari walikuwa mashahidi wa kile wanasheria wa makosa ya jinai wanachokiita crime rate, kukua kwa kiasi cha kutisha.

Hata hivyo, mwaka 1998 Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania lilitunga sheria inayoitwa Sheria Maalumu ya Makosa ya Kujamiiana au kwa lugha ya kigeni ‘Sexual Offences Special Provisions Act’ au kwa kifupi SOSPA.

Sheria hii ilitiwa saini na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa wakati huo, Benjamin Mkapa Julai mwaka 1998.

Kwa kiasi kikubwa sheria hii ilikuwa kama shubiri wa tatizo la makosa ya kujamiiana kama ubakaji au kufanya ngono kinyume cha maumbile katika jamii yetu.

Leo tutaiangalia sheria hii, yaliyomo, adhabu zake na mabadiliko katika sheria hii.

Kwa kiasi kikubwa, sheria hii imekuja kufanya mabadiliko katika sheria kadhaa za makosa ya jinai kama vile Kanuni ya Adhabu (sura ya 16 ya sheria za Tanzania) Sheria ya Ushahidi na Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Hivyo sehemu ya kwanza ya sheria hii imefanya mabadiliko katika sheria ya kanuni za adhabu.

Ndani ya sheria hii mvulana ametambuliwa kama mwanamme aliye chini ya miaka 18.

Hii ina maana kwa mtoto wa kiume kutambulika kama mtoto, umri wake ni lazima uwe chini ya miaka 18, wakati kwa msichana, yeye ametambulishwa kama mwanamke aliye chini ya miaka 18 pia.

Chini ya kifungu cha 4 cha sheria hii, kanuni ya adhabu imefanyiwa marekebisho na kwa sasa kwa mtoto ambaye ‘hajakomaa’ (immature) umri wake ni ule ulio chini ya miaka 10.

Kisheria, mtoto huyo hawezi kuwa na mashitaka wala hatia ya makosa ya jinai hata hivyo, marekebisho yaliyofanyika kwenye kifungu kidogo cha 2 cha kifungu cha 15 cha kanuni za adhabu, kinaelekeza kwamba mtoto aliye chini ya miaka 12 hawezi kuwa na hatia ya kosa la jinai isipokuwa kama wakati anatenda au anaacha kutenda tendo (ambalo ni jinai), itathibitishwa kwamba alikuwa na uwezo wa kujua kwamba hatakiwi kutenda au kutokutenda kosa hilo.

Pia kifungu hiko kinamtoa hatiani kwa kosa lolote la jinai mtoto wa kiume aliye chini ya miaka 12 kwa dhana kwamba hawezi kufanya tendo la ngono, kubaka.

Tofauti na wengi wanavyodhani kwamba kubaka ni tendo la kumlazimisha mwanamke kufanya mapenzi, sheria hii imetoa maana pana ya neno kubaka.

Chini ya kifungu cha 5 cha sheria hii, ambacho kimetengeneza kifungu cha 130 cha Kanuni za Adhabu inasomeka kwamba kubaka ni kitendo cha mtu mwanamme kufanya tendo la ndoa na mwanamke bila idhini au kitendo cha kufanya tendo la ndoa na mwanamke ambaye si mke wake au mke wake lakini waliye tengana naye na bila idhini yake; au kwa idhini yake ambayo imepatikana kwa kutumia nguvu, vitisho.

Au kwa kuweka maisha yake katika hofu ya kifo, kuumia, akiwa katika kifungo au kwa idhini yake lakini idhini hiyo ikiwa imepatikana akiwa katika akili iliyochanganyikiwa kama amelewa kwa dawa aliyopewa na mwanamme huyo, isipokuwa endapo itathibitika kwamba kulikuwa na makubaliano awali, mwanamme atahesabika kuwa amebaka kama atafanya tendo la ndoa na msichana aliye chini ya miaka 18 hata kama msichana huyo atakuwa amekubali kufanya tendo la ndoa kwa ridhaa yake.

Pengine kwa kutambua kwamba kuna aina nyingine za ubakaji, sheria hii chini ya kifungu cha 5 kifungu kidogo cha 3 imetoa maana nyingine zaidi ya kubaka kwa kujumuisha maana hiyo kwa kitendo cha mtu mwenye mamlaka katika ofisi anapofanya tendo la ndoa na mtu wa chini yake kimamlaka au pale ofisa mahabusu zilizoanzishwa kisheria atakapofanya ngono na mahabusu mwanamke.

Maana nyingine ya kubaka ni pale maofisa wa afya au hospitali watakapotumia mwanya wa nafasi zao kufanya tendo la ndoa na mgonjwa msichana au mwanamke; au kwa waganga wa tiba za jadi atakaye tumia mwanya wa nafasi yake kufanya tendo la ndoa na wagonjwa wake wa kike, mtumishi wa dini ambaye kwa kutambua ushawishi wake juu ya waumini wake afanye nao ngono nao (waumini wanawake).

Kosa la shambulio la aibu litahesabika tu pale ambapo mtu akiwa na nia ya kusababisha aibu ya kingono kwa mtu yeyote.

Neno lolote, sauti yoyote, ishara yoyote au kuonekana kwa picha yoyote ikimaanisha sauti mdhaliliko wa kijinsia, atakuwa na hatia ya kufanya shambulio la aibu na kwa adhabu atahukumiwa kwanda jela kwa kipindi kisichozidi miaka mitano (5) au faini isiyozidi sh 300,000 au vyote, jela na faini kwa pamoja.

Lakini kama shambulio hili la aibu linahusisha msichana aliye chini ya miaka 18, mtuhumiwa hawezi kujitetea kwamba msichana huyo aliridhia shambulio hilo.

Katika mitaa yetu, baadhi ya mambo yanakemewa vikali na sheria na bado yanapata nafasi, ikiwamo watu kutumia lugha za kudhalilisha kimapenzi watu wengine.

Tunapaswa tujue kwamba haya ni makosa ya jinai na ni lazima hatua za kisheria zichukuliwe ili kuyakabili kama si kuyatokomeza kabisa.

Biashara ya ukahaba

Kosa jingine ambalo sheria hii imelielezea ni lile kosa la kufanya ukahaba.

Hili nalo ni kosa la jinai chini ya kifungu cha 12 cha Sheria ya Makosa ya Kujamiiana, ambacho ni marekebisho ya kifungu cha 139 cha Kanuni za Adhabu.

Kuna sababu au visingizio mbalimbali ambavyo watu wengi hasa mijini wanavitaja kama ndiyo sababu zinazosababisha jinai hii kutendeka, lakini ukweli ni kwamba biashara ya ukahaba imeshamiri sana.

Pamoja na sababu au visingizio vinavyotolewa na watu mbalimbali juu ya kufanya biashara hii, lakini katika upande wa sheria, hili ni kosa la jinai na adhabu yake imeanishwa katika kifungu cha 139 ni kifungo kisichopungua miaka 10 jela na faini isiyopungua sh 100,000 na isiyozidi sh 300,000 au vyote faini na kifungo kwa pamoja.

Usafirishaji wa binadamu

Pamoja na makosa yaliyotajwa hapo juu, kuna kosa lililoorodheshwa kama kosa la kusafirisha binadamu.

Hili limetambuliwa chini ya kifungu cha 139A kama kilivyorekebishwa na kifungu cha 14 cha sheria hii.

Ndani ya kifungu hiki , mtu yeyote atakaethibitika kwamba anatangaza, anasaidia au anapigia upatu kununua au kuuza au kubadilishana mtu yeyote kwa ajili ya kupata pesa au malipo mengine, iwe ndani au kwa nia ya kusafirisha mtu huyo nje ya Jamhuri ya Muungano, bila idhini ya wazazi au waangalizi wake; au akipata idhini ya mwanamke mjamzito kwa ajili ya pesa na kumuasili mtoto wa mwanamke huyo ambaye hajazaliwa.

Au anawasaidia wanawake hao kupata ujauzito kwa nia ya kuzaa au kama anahusika na usajili wa vizazi, akijua na bado akaruhusu kutoa taarifa zisizo sahihi juu ya uzazi wa wowote au akisajili taarifa zisizo sahihi, pia atakuwa na hatia ya kutenda kosa la kusafirisha watu na adhabu yake ni kifungo si chini ya miaka 20 na kisichozidi miaka 30 na fidia isiyopungua sh 300,000 au vyote, jela na faini kwa pamoja.

Kiasi hiki hata hivyo, kitaamuliwa na mahakama.

Kanali Gaddafi: Roho ya maskini wa Afrika inayokaribia kung'oka

KANALI Muammar Gaddafi ni kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika na katika nchi za Kiarabu.
Ameongoza Libya tangu alipompindua Mfalme Idris I, katika mapinduzi yasiyo ya kumwaga damu, wakati huo akiwa na umri wa miaka 27.
Maarufu kwa nguo anazopenda kuvaa, na walinzi wa kike wenye kubeba silaha, kiongozi huyo wa Libya pia anadhaniwa kuwa na mbinu nzuri za kisiasa, kwa kuweza kuirejesha Libya kutokana na kutengwa kidiplomasia duniani.
Baada ya miongo miwili ya kutengwa katika jamii ya kimataifa, mwaka 2003, Tripoli ilikiri kuwa walifanya shambulio la Lockerbie kwa kuiangamiza kwa mabomu ndege ya Pam Am na hapo Umoja wa Mataifa ukaondoa vikwazo dhidi ya Libya.
Baada ya miezi kadhaa, serikali ya Kanali Gaddafi ilisitisha mipango yake ya kuunda silaha za maangamizi na hiyo ikarejesha ushirikiano na nchi za magharibi.
Hapo ndipo mabadiliko halisi yalionekana kwa kuwa nchi hizo za magharibi zilibadili mtazamo wao na kuacha kumtenga Gaddafi na kushirikiana naye hata kama alikuwa hatabiriki.
Ni mtu wa kipekee katika kauli zake, mienendo yake, tabia zake na mikakati yake, kwa mujibu wa Saas Djebbar mtaalam wa siasa za Libya.
“Lakini ni mwanasiasa mashuhuri; hakuna shaka lolote kuhusu hilo. Ni mwanasiasa anayeweza kuhimili misukosuko ya kisiasa kwa hali ya juu sana.”
Muammar Gaddafi alizaliwa jangwani karibu na Sirte mwaka 1942.
Alipokuwa kijana alivutiwa na kiongozi mzalendo wa Misri, Gamal Abdel Nasser, alipokuwa akishiriki katika maandamano dhidi ya Israel wakati wa mtafaruku wa Suez mwaka 1956.
Gaddafi alipanga njama ya kupindua utawala wa kifalme alipokuwa mwanafunzi wa kijeshi na aliwahi kupata mafunzo zaidi akiwa Uingereza kabla ya kurejea nyumbani Libya, mji wa Benghazi, na kupanga mapinduzi ya Septemba 1 mwaka wa 1969.
Ghaddafi alianza kujenga itikadi zake za kisiasa mwaka 1970 na kuziandika katika kitabu chake cha kijani kibichi.
Alikitumia kitabu chake kuanzisha mfumo wa kisiasa iliyojumuisha kanuni za kiislamu na mfumo uliyo tofauti na siasa za ujamaa au ubepari.
Mwaka 1977 aliasisi mfumo ujulikanao kama 'Jamahiriya' au 'Taifa la Umma' ambapo raia ndio wanaoendesha uongozi wa nchi yao kupitia 'kamati za umma'.
Mfumo huo wa Gaddafi umevuka mipaka na hauhusishi mambo ya siasa tu, bali pia mambo mengine.
Akiwa safarini ng'ambo, huwa anakaa kwenye kambi iliyojengwa kwa mahema yake ya kifahari ya Kibeduwi akiwa amefuatana na walinzi wanawake ambao, inasemekana, huwa hawapotezi umakini kazini kama walinzi wanaume.
Hema hiyo pia hutumiwa kuwalaki wageni wa Libya na Kanali Gaddafi huendesha mikutano na mahojiano yake humo humo akipepea usinga au tawi la mitende.
Benjamin Barber, mtaalam wa kisiasa wa kujitegemea, kutoka Marekani amewahi kukutana na Gaddafi mara kadhaa hivi karibuni na kuzungumza naye kuhusu mustakabali wa Libya.
Barber alisema Muammar Gaddafi anajihisi kuwa msomi aliyebobea.
Muammar Gaddafi na Tony Blair waliwahi kuandaa mkutano wa viongozi kutoka nchi mbalimbali Mei 29, 2007 kwenye hema hiyo ya Kibedui.
"Utashangazwa kuwa ingawaje ni dikteta, ni mwanafalasafa na mwenye kutafakari jambo kabla ya kuzungumza," aliiambia BBC.
"Namchukulia sana kama mtu kutoka kabila la Waberber na mtu ambaye aliibuka kutoka tamaduni za watu wa jangwani, kutoka kwenye mchanga na kwa namna fulani kuna tofauti kubwa na uongozi wa kisasa, na kwa namna fulani hilo limemfanya awe mstahamilivu na mwenye msimamo."
Kanali Gaddafi amejitahidi kwa muda mrefu kutoa ushawishi wake nyumbani na ng'ambo.
Awali alituma jeshi lake nchini Chad ambapo wanajeshi walidhibiti ukanda wa Aozou, kaskazini mwa nchi hiyo, mwaka 1973.
Katika miaka ya 80 aliandaa mafunzo kwa makundi ya waasi kutoka Afrika Magharibi yaliyojumuisha wale wa Tuareg ambao ni Waberber.
Hivi karibuni aliongoza jitihada za kuwapatanisha waasi wa Tuareg kutoka nchi za Niger na Mali.
Jumuiya ya wanadiplomasia kuitenga Libya kulitokana na Kanali Muammar Gaddafi kuunga mkono makundi yeneye silaha, ikiwemo Irish Republican Army na Palestine Liberation Organisation, PLO.
Rais wa zamani wa Marekani, Ronald Reagan alimwita Gaddafi 'mad dog' yaani 'mbwa kichaa' na Marekani ililipiza kisasi dhidi ya Libya kwa madai ya kuhusika na mashambulio ya anga barani Ulaya kwa kuvamia miji ya Tripoli na Benghazi mwaka 1986.
Ilisemekana kuwa Kanali Gaddafi alitikiswa na mashambulio ya mabomu hayo ambapo mtoto wake wa kike wa kufikia aliuawa.
Aliposhindwa katika jitihada zake za kuzipatanisha nchi za Uarabuni katika miaka ya 90, Kanali Gaddafi alielekeza nguvu zake barani Afrika na kupendekeza 'Muungano wa Nchi' za bara la Afrika.
Alianza kuvaa mavazi yake binafsi, sare za michezo zilizo na ngao za bara la Afrika au picha za viongozi kutoka bara hilo.
Wakati wa mabadiliko katika karne ya 20, huku Libya ikiwa inapata tabu kutokana na vikwazo dhidi ya nchi hiyo, alianza kurekebisha hali nchini mwake.
Mwaka wa 2003, mabadiliko yakaanza kuonekana na baada ya miaka mitano mkataba wa kulipa fidia kwa waathirika wa Lockerbire uliafikiwa na hii ikarejesha uhusiano kati ya Washington na Libya.
“Hakutakuwa na vita tena, mashambulio, na vitendo vya ugaidi,” Kanali Gaddafi alisema alipokuwa akisherehekea miaka 39 aliyokaa madarakani.

Kiongozi huyo wa Libya hujiona kama kiongozi wa kidini wa taifa hilo, akihakikisha kwa kile anachosema ni demokrasia.
Lakini katika hali halisi, wakosoaji wanasema Kanali Gaddafi amefanikiwa kudhibiti nchi hiyo.
Wanaompinga wanasema wamekandamizwa kikatili na vyombo vya habari vinabaki katika udhibiti mkubwa wa serikali.
Libya ina sheria ambazo haziwaruhusu watu kukusanyika katika misingi ya kisiasa zinazopinga mapinduzi ya Kanali Gaddafi.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema serikali hiyo imewatia mbaroni mamia ya raia kwa kukiuka sheria hiyo na baadhi yao kuhukumiwa kifo.
Imeripotiwa kumekuwa na matukio ya utesaji na hata watu kupotea
Inadhaniwa kuwa Kanali Gaddafi anaandaa namna ya kukabidhi madaraka yake kwa sababu ya umri aliyofikia sasa lakini haijulikani ni nani atakayerithi uongozi wa Libya kutoka kwa Gaddafi.
Kuna hisia kuwa mwanawe Sayf Al-Islam Gaddafi ndiye atarithi uongozi kutoka kwa baba yake na anaongoza katika kuleta mabadiliko.
Ingawaje Sayf ametangaza kuwa anastaafu siasa lakini kuna wanaohisi kuwa hiyo ni mbinu ya kuongeza ushawishi wake kisiasa.
Wakati huo huo, Gaddafi ameahidi kuwa wizara za nchi hiyo zitafutwa pamoja na bajeti zao
Utajiri utakaopatikana kutokana na mafuta utakabidhiwa moja kwa moja kwa wananchi.
Licha ya uchumi wa Libya kutoa fursa kwa wawekezaji wa nje, mabadiliko bado yanakwenda taratibu.
Walibya wengi wana wasiwasi juu ya mabadiliko yanayotokea na kuhisi kuwa hawapati manufaa kutokana na rasilmali ya Libya, waangalizi wanasema kwani huduma za serikali ni duni pamoja na ubadhirifu mkubwa wa mali.
“Wanajihadhari sana katika mapambano hayo kwa kuwa hawataki mabadiliko yatakayolegeza nguvu za umma,” alisema Saad Djebbar
“Lakini wakati huo huo, Walibya wanafahamu kuwa wanahitaji kufanya mabadilko. Na ndio maana wanaenda taratibu sana.